HOTEL YA KWANZA KWA UBORA DUNIANI IPO TANZANIA. Hoteli ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania, inathibitisha kufuru ya utajiri uliopo Tanzania. Singita ndiyo hoteli nambari moja duniani, ikichukua tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na taasisi maarufu ya Marekani, US Travel + Leisure ambayo ‘hudili’ na viwango vya biashara ya utalii duniani. Hoteli hiyo, inathibitisha kwamba thamani ya Tanzania ipo juu mno, ndiyo maana mwekezaji kutoka Afrika Kusini, Luke Bailes, aliamua kufanya uwekezaji wa hali ya juu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Matokeo hayo, yaliandikwa Agosti mwaka huu kwenye jarida maarufu kwa kuchapisha matukio ya biashara za utalii, linaloitwa T+L Magazine. Jarida hilo linamilikiwa na Taasisi ya US Travel + Leisure. Tangu kufunguliwa kwake, Singita Grumeti imekuwa kivutio cha viongozi, matajiri na watu maarufu ambao mara kwa mara hutinga kujivinjari, vilevile kujionea vivutio vya utalii vilivyop...