Bil 280 zitamfanya Cristiano Ronaldo avue jezi ya Real Madrid na kuhama Spain?


Bil 280 zitamfanya Cristiano Ronaldo avue jezi ya Real Madrid na kuhama Spain?

C Ronaldo IIZiliwahi kukaa story kwenye magazeti na mitandao mikubwa ya habari duniani kwamba staa wa soka, mrenoCristiano Ronaldo atarudi kuichezea klabu yake ya zamani, Man United.. ikapita muda hilo halikutokea.
Imekuja nyingine, tayari imeanza kuchukua headlines kwamba Ronaldo ataondoka Madrid, safari yake inakuwa kwenda wapi? Mezani dau limewekawa kiasi gani? Majibu niko nayo tayari.
C RonaldoPSG offer €125 for Ronaldo”—kichwa cha habari chenye wino mzito kwenye gazeti la michezo la Madrid, Hispania… story ndani ni kwamba Klabu ya PSG ya Ufaransa wametangaza dau la Euro Mil. 125 (sawa na kama Bil. 280 hivi) kwa ajili ya kumvuta staa huyo ajiunge na kikosi chao japo mwenyewe bado hajatolea majibu kuhusu ishu hiyo.. tetesi nyingi za ishu za soka mara nyingi zinakuwa na chembe chembe za ukweli hivi, na hii je?
Story nyingine inasema staa huyo ni kama hayuko tayari kuondoka Madrid mpaka mkataba wake utakavyoisha msimu wa 2017/18.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

List ya washindi wote #BillboardAwards2015.. Pichaz za mastaa wote Red carpet

HOTEL YA KWANZA KWA UBORA DUNIANI IPO TANZANIA.

rangi za nguo zinazofaa kuvaliwa Siku Ya usaili