HUU UTANI MWINGINE UNAWEZA UKARUSHA NGUMI, ANGALIA PICHA ALIVYOFANYWA IKER CASILLAS


HUU UTANI MWINGINE UNAWEZA UKARUSHA NGUMI, ANGALIA PICHA ALIVYOFANYWA IKER CASILLAS

SARE ya 1-1 waliyopata Real Madrid kipindi cha pili jana usiku Santiago Bernabeu inaweza kuhitimisha safari ya soka ya Iker Casillas.
Casillas, aliye kwenye kiwango kizuri msimu huu aliokoa michomo ya hatari iliyopigwa na  Claudio Marchisio na Paul Pogba.
Juventus walifunga goli la kusawazisha kipindi cha pili kupitia kwa Alvaro Morata.
Mlinda mlango gwiji wa Hispania pia aliungana na wachezaji wenzake kushambulia, lakini dakika ya 93 alizua kituko baada ya kupata mpira wa kurusha.
Casillas alichukua mpira haraka na kutaka kumrushia Marcelo, lakini alisahau sheria za mpira wa miguu katika urushaji wa mpira.
Mpira haukuvuka kichwa cha Casillas na mwamuzi Jonas Eriksson akaamuru iwe adhabu na Juventus wakapewa nafasi ya kurusha baada ya kipa huyo kuchemsha.
Na hapo ndipo ndoto za Real Madrid zikazima na kama Iker Casillas angefanikiwa kusababisha goli ingekuwa historia kubwa katika maisha yake ya soka.
Kama kawaida, Internet imefanya kazi yake kama wengi walivyotarajia ambapo watu wametengeneza picha kumkejeli Casillas....Angalia picha chini
Screen Shot 2015-05-14 at 09.58.39
Screen Shot 2015-05-14 at 09.57.02
Screen Shot 2015-05-14 at 09.55.40

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

List ya washindi wote #BillboardAwards2015.. Pichaz za mastaa wote Red carpet

HOTEL YA KWANZA KWA UBORA DUNIANI IPO TANZANIA.

rangi za nguo zinazofaa kuvaliwa Siku Ya usaili