Machapisho

Tayari Edward Lowassa kaingia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ninazo pichaz nyingine hapa

Picha
Tayari Edward Lowassa kaingia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ninazo pichaz nyingine hapa Ninayo Ripoti nyingine toka Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Arusha , watu walianza kuingia toka saa moja asubuhi. Mbunge  Edward Lowassa  tayari kaingia Uwanjani, kinachosubiriwa ni hotuba yake. Kulikuwa na mvua ndogo hivi lakini watu wameendelea kuingia, mpaka sasa hii Uwanja umejaa, watu ni wengi na wapo baadhi ya viongozi mbalimbali ambao tayari wamefika ikiwemo  Mzee Kingunge .